Y Jay Tishio La Kusini ,Anatarajia Kudondosha Kishindo Kikubwa Wadau Wamtabiria makubwa.




Msanii wa Mziki wa Bongoflava Kutoka Tanzania maarufu kama Y Jay Ameamua kuweka wazi mipango ya kuachia ngoma mpya itakayo mvusha katika mziki wa Bongo Flava na kutambulika kimataifa zaidi.Kwasasa amesema anataka kufanya callable na msanii mkubwa ambayae anafanya vizuri katika game la mziki hapa nchini amesema muda ukifika ataweka wazi  ni msanii gani ambaye atamshirikisha.

Kuhusu Studio amesema kuwa anatarajia kufanya na  mtayarishaji wa mziki ambaye anaanda ngoma nyingi za Jux moja kwa moja watu wametafsiri kuwa atakuwa ni Bob Manecky kutoka Am Records ikiwa ni producer mkubwa ambaye anafamya vizuri na ametengeneza ngoma nyingi za Jux.

Pia amewashukuru wadau wake kwa kumpa support kubwa tangu ameachia ngoma yake ya show love ambayo inafanya vizuri mpaka hivi sasa mtandaoni na kwenye Radio pamoja na Tv.Ikiwa amesema kuwa huu sio Muda wa kushinda kufanya kazi kwa wasanii wa kusini bali ni muda wa kufanya kazi nzuri kwaajili ya watu wazuri ambao wanapenda mziki na kazi za wasanii.

Baada ya Radio mmoja hapa Jijini Dar es salaam Kupiga stori na meneja wake y jay ambaye hajataka jina litajwe ikiwa ipo siku atajiweka wazi maarufu kama Kadefu amesema huu ni Mwaka wa kutoa ngoma kali tu na sio maneno ni kazi juu ya kazi wadau wa y jay wakae mkao wa kula.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment