Msanii wa Bongo flava ambaye ameweza kuishi kwa muda mrefu katika Game Bila ya kupotea kama wasanii wengine,Na hapa namzungumzia Matonya Ambaye kwa mara ya Kwanza wakati yupo Jijini Tanga alianzisha kundi la Hard boyz family kundi ambalo lilikuwa na wenzake kadhaa ambao walikuwa wanaunda kundi hilo,
Akizungumza na MwakaTV ameeleza sababu ya yeye kuitwa matonya nikutokana na hatua alizopitia katika utafutaji wake kuingia mtaani na kuanza kuomba hela kwa washikaji ili aingie Studio kurekodi Ngoma na washikaji wakimuona basi walikuwa wanamtania kwa kusema ''Matonya huyo anakuja''Kutupiga mzinga.
Lakini kutokana na Uwezo aliokuwa nao matonya Washikaji hawakusita kumpa fedha itakayo msaidia kuingia studio kurekodi nyimbo ndipo watu wakaanza kuufahamu uwezo wa Matonya katika Mziki huu.
Matonya ni msanii ambaye amekuwa na sifa kubwa ya uandishi mzuri wa mashairi katika ngoma zake hasa za mapenzi na sasa amekuwa Gumzo kubwa baada ya kuachia ngoma yake mpya ya ''Sugua Benchi''ambayo tayari ameshaachia na video yake.Ikiwa ni Ngoma ambayo inafundisha sana kitaa bila karamu wa daftari ni kwa kusikiliza mashairi tu.
Never Give Up ,Bring it On
Home / Uncategories / Hitmaker wa Sugua Benchi Matonya Kumbe Jina la Matonya Alilipata kutokana na Tabia ya Kuomba Omba Looh,Lakini sasa Ni kioo cha Jamii
Blogger Comment
Facebook Comment