Miss Namba Mbili Njombe Naila Ally safarali Kukutana na Mwanamitindo Maarufu Hamisa Mobetto


Aliyekuwa Miss NambaMbili Mkoa wa Njombe 2016  Naila Ally safarali maarufu kwa Jina la Naylove amefunguka kuhusu malengo yake na management ya MKclassic inayomsimamia kazi zake,Ameeleza mipango mikakati ya uongozi wake Chini ya Meneja wake Emmanuel Mnami kuwa uongozi unampango wa kumkutanisha na Hamisa Mobetto ambaye Ni mwanamitindo Maarufu Afrika,

 Naylove katika picha 
Amezungumza hayo hivi karibuni wakati akifanya Media Tour Hapa Jijini Dar es salaam kuwa anashukuru uongozi wake kwa kumuamini na kumfikisha mpaka hapa alipo kwa kufahamiana na wasanii na wanamitindo mbali mbali ambao wamekuwa wakimpa changamoto kubwa katika kufanikisha malengo yake aliyoyapanga ili kuitambulisha Njombe katika Ramani ya Dunia kwa kutangaza vivutio vyote ambavyo vinapatikana Mkoani Njombe hata Tanzania kiujumla.

Akizungumzia kuhusu taarifa za kuvishwa pete kama taarifa zilivyoenea kwenye Mitandao ya Kijamii Amesema Kuwa Alijikuta amepost taarifa za kuvishwa pete ingawa bado hajavishwa ikiwa ni moja ya Malengo yake.

Mwisho ameeleza kuwa Mwezi wa kumi na mbili atajiunga katika Mashindano makubwa ya Mitindo Tanzania yatakayofanyika mwaka huu huku akiwashukuru wadau wake na wazazi wake kwa msaada wanaompa  
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment