Wasanii Wawili Wanaounda Kundi La Eagle Eyes Kutoka Njombe Maninga Martin Nalitote na Brass T Kilasi Wamewashitua watu baada ya Kuonekana Wakijianda Kwa Maandalizi makubwa ya Kufunga Mwaka Kwa Mambo Makubwa hii ni baada ya Kufungua Rasmi Akaunti yao ya Youtube kwaajili ya Kuachia Video zao hivi karibu,Wamezungumza hayo wakati wakifanyiwa Mahojiano na Radio Magic fm jijini Dar es salaam
Baada ya wasanii Wa Njombe Baadhi yao Kuwalaamu na Kusema kuwa Wamefail katika mziki wa Bongo Flava Wametoa Kauli ambayo Imeonekana kama imewakera wasanii wengi kutoka mkoa huo baada ya kundi hilo kusema wanamtazama msanii kama Diamond na hawaoni wa kufanishwa na msanii yeyote kutoka Njombe.
Hata hivyo wameeleza mipango yao na ukimya wao Wamesema kuwa Ni kutokana na majukumu mbali mbali ya kimaisha yaliwafanya wakae kimya,Huku wakisema mipango yao ni kuachia Nyimbo Tatu kuanzia hivi sasa huku ngoma ya kwanza wadau wao wakae mkao wa kula kuanzia Hivi sasa.
Pia wametupa kijembe kwa wale wote wanaosema kuwa Kundi hili haliwezi kufika mbali kuwa wakae na mawazo yao finyu lakini wao watazidi kufanya vitu vizuri kwaajili ya wadau wao,Kundi hili lilitamba na ngoma kama ''nisubirie''
Home / Uncategories / Eagle Eyes Kutoka Njombe Macho yao Yamtazama Diamond na Wasanii wakubwa Wa Kimataifa,Njombe Hakuna Wa Kuwatisha,
Blogger Comment
Facebook Comment