Msanii wa Filamu Na Muimbaji Wa Mziki wa Bongo Flava BMK Theoneste Amejipanga Kufanya Makubwa katika Filamu Tanzania

Msanii Anayefanya vizuri katika kiwanda cha filamu Bmk Theoneste Ameweka wazi mipango mikakati ya Kuifanya Tanzania kuwa Katika ramani ya Mpya ya Filamu Tanzania kwa Kuunda kundi ambalo bado hajalipa jina  litakalo husika na Kufanya Filamu za aina mbali mbali katika kuelimisha Jamii na kuburudisha jamii,Ambapo yeye ameamua kutumia mazingira ya Tanzania ili kuitangaza Tanzania hata katika swala zima la Utalii wa Ndani.


Amezungumza hayo wakati akifanyiwa interview na Mwakatv kuhusu Filamu yake Mpya ambayo ambayo amepanga kuifanya  itakayo washiirikisha mastaa mbali mbali kutoka Tanzania,

Hata hivyo amefurahishwa na hatua ambayo mziki wa Bongo Flava Tanzania umefikia na angefurahi kuona Kasi ya wasanii wa filamu kutoka Tanzania wanashiriki katika Tuzo Kubwa Dunia na hayo yote yanakuja kwa Kuweka ushirikano kati ya wasanii wenyewe wa filamu na wadau.

Kuhusu ujio wa Ngoma yake amesema tayari wameshashoot na siku yeyote kuanzia leo ataiachia mtandaoni, Na Mwisho amewashukuru wadau kwa kumpokea katika sanaa anayoifanya.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment