Imekuwa ikitokea mara kwa mara watu kutokujiamini, kutokana na mapungufu au ulemavu wa aina mbali mbali.
Shabiki mdogo wa rapper Fetty Wap, ambaye alizaliwa na tatizo la kutokuona jicho moja ( retinoblastoma) amehamasika kwenda shule baada ya kumuona Fetty akiwa na tatizo hilo pia.
Mama wa kijana huyo Brenda Vaden, ametumia Instagram akaunti yake kumshukuru rapper huyo wa New Jersey, kwani kijana wake awali hakuwa akitoka nje wala kwenda shule.
“Asante kwa Fetty wap kwa kumpa mwenetu Jayden, kitu ambacho hatukuweza ‘kujiamini’, asante sana Wap kwa kubadilisha maisha ya Jayden umerudisha furaha yake tena” ameandika mama huyo.
Rapper huyo akatumia time kumjibu mama Jayden.
“Ninachotaka ni kuonesha dunia kwamba, haijalishi unamuonekano upi, aijalishi uko vipi, jaribu kujiamini na kutembea kifua mbele, kwamba unaweza kufanya chochote, asante Jayden kwa kujiamini na asante kwa kuwa shabiki wangu” ameandika Fetty Wap.