Msanii Wa Nyimbo Za Injili Aline Vyuka Ajiandaa Kuachia Album Mpya.Ni Mwendo wa Kuitangaza Injili,

Baada ya Ngoma Yake ya ''Jinsi Nilivyo''kufanya Vizuri Katika mziki wa Injili Huku akiwa amekaa kimya kwa Muda mrefu Msanii Aline Vyuka amejipanga Kuachia Album nyingine itakayokuwa na nyimbo zaidi ya Tano huku akieleza mikakati yake ya kuitangaza na kueneza Injili kwa njia ya Nyimbo.
                       Aline Vyuka Katika Pozi na Hisia za Kusifu

Hata hivyo amesema kuwa Ukimya wake ulitoka na mambo mbali mbali ya kifamilia Huku akielezea album yake itakayotoka na Video ambayo Location ya imepengwa kufanyika Bagamoyo,Zanzibar na Kigamboni.

Tanzania wanamfahamu Aline Vyuka kama msanii ambaye anatunga mashahiri Vizuri na Sauti yake nzuri pindi atakapomwimbia Bwana kwa Pambio,Ni msanii ambaye anaishi nchini Marekani Huku akifurahia Mziki wa Injili kwa sasa Unapofanya Vizuri,

Pia amewataka wadau wake wakae mkao wa kula kwaajili Ya Nyimbo nyingi na zenye Ujumbe Mzito

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment