Msanii Wa Filamu Ambaye Pia Ni Director na Producer Kutoka Mkoa wa Mjombe Ramadhani Shomari Maarufu kwa Jina la Ram Shomy azungumzia Filamu yake ya Mshenga na Kueleza mambo mbali mbali ambayo anayafahamu katika kiwanda cha Filamu Tanzania huku akieleza changamoto mbali mbali ambazo zinaikumba Tasnia hiyo.
Ram Shomy
Amesema kuwa Yeye kama msanii na mtayarishaji wa filamu hapa nchini amesema kuwa Tatizo kubwa ambalo limekuwa ni kilio kikubwa tangu siku nyingi ni Uwizi wa kazi Za Sanaa Hii amesema nitatizo kubwa ambalo linawavunja moyo wasanii wengi katika kiwanda hicho huku wakitumia gharama kubwa katika maandalizi yao.Hivyo ameiomba serikali kupitia kwa Waziri Wa Michezo,Sanaa na Utamaduni Mwenye Dhamana Kutoa mchango katika hili janga lakini huku akifurahia jitihada ambazo amezifanya Tangu apate Dhamana hiyo.
Pia amewaweka wadau wake kuwa tayari kwa mambo makubwa ambayo atayafanya Mwishoni mwa Mwaka huu ikiwa na kuongoza Video kubwa zitakazo washirikisha Wadau wakubwa na wasanii wakubwa hapa nchini,Huku akisisitiza Wadau wake kuitazama Mshenga Madukani masaa 24
Blogger Comment
Facebook Comment