Muonekano Mpya wa Mwakatv.blogspot.com na Mipango yake ya Mwaka TV,Kumbe si kwaajili ya wasanii wa Mkclasic tu ni ya wote?

Mkurugenzi wa Blog Hii Immanuel Mwakapotela Maarufu kama Mwaka Ze Bwoy  mtangazaji wa Channel ten tv na Mwanzilishi na Mmiliki wa kampuni ya Mkclassic, Ambaye Pia alikuwa  ni Mtangazaji wa Uplandsfm Iliyopo Mkoani Njombe,Ameonyesha Muonekano Mpya wa blog yake anayomiliki kwa kuweka muonekano mpya na wenye kuvutia kama  unavyoonekana katika hii Picha hapa chini.

  Muonekano Mpya Wa Blogs Ya Mwaka ze Bwoy ambayo ni Mwakatv.blogspot.com
Kwa upande mwingine amewashukuru wote waliofanikisha zoezi hili ambao ni Clement Silla,Boysella,Colimba INC,John Brudda na Wengine Kwa Kufanikisha Mchakato Huu,Huku akifurahia Uwepo Wa Fast Jet Ambao Ni wasafirishaji wa abiria kwa njia ya anga yaani ndege kuelekea sehemu mbali Tanzania.

Lakini pia ameeleza kuhusu kuwapendelea wasanii wanaomilikiwa na kampuni yake ya Mkclassic amesema hii ni blog ya Watu wote kila mmoja inamhusu na  watu wa nje ya Mkclassic  na hata wasanii wa Mkclassic na Meneja wao Immanuel Mnami wakileta Tangazo au chochote cha kulipia Watalipia tu kwasababu hii ni ofisi inayojitegemea ingawa Mkurugenzi ni mmoja.
 ''Nashukuru Mungu kwa hatua hii ambayo nimeifikia hapa naamini kila jambo linawakati wake na linatendeka kwa Muda maalumu na sasa niliwaahidi wadau wangu kuwaletea habari katika muonekano mzuri na sasa muda umefika kazi kwao,lakini naomba niweke wazi hii ni blog ya watu wote si kwaajili ya wasanii wa mkclassic''amesema mkurugenzi Mwaka ze bwoy

Kuhusu kuwapa support sana wasanii wa Njombe ameweka wazi kuwa Ni wasanii ambao anawafahamu toka muda mrefu kwahyo anaukaribu nao mkubwa na anawafahamu kwa uwezo wao na ndiomana ameanza nao hao ila hata mikoa mingine wanakaribishwa na atasaidiwa tu,

Amesema pia kwa sasa Mkclassic inawasanii Wawili na Mwanamitindo mmoja wasanii ni Brana Radium na Sajo Mabusness huku Mwanamitindo ni Naylove  wote ni kutoka Mkoa wa Njombe Ikiwa kwa sasa Kampuni inampango wa kumuongeza msanii wa kike na Mwanamitindo mwingine.

Endelea kufurahia muonekano wetu
Aidha amewaomba wadau kufuatilia MwakaTv Ambayo inapatikana katika hii Blog yako kwaajili yako mdau unayeifatili ili kupata habari mbali mbali na Ngoma mpya za kila siku

Nakusogeza karibu na picha za Mkurugenzi wa Hii Blog Mwaka ze Bwoy



  Mwaka ze bwoy akiwa Ofisini Channel ten tv
Mkurugenzi wa hii blog na mmiliki wa Mkclassic Mwaka ze boy  katika pozi
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment