
Aliyehukumiwa kutumikia kifungo hicho ni Samwel Mnyonge (30) ambapo
hukumu hiyo imetolewa na hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya
Mbarali, Guwai Sumaye.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi,
Mazoya Luchagula mbele ya hakimu mfawidhi Sumaye kuwa mshitakiwa
alitenda kosa hilo Februari 11, 2014 kijijini Madibira.
Alisema awali mshitakiwa alimbeba mtoto huyo wa umri wa miaka mitano
kwenye baiskeli akiwa amempa msaada wa kumrejesha nyumbani alipokuwa
akitokea shuleni, lakini wakiwa njiani, Mnyonge alimpeleka mtoto kwenye
shamba la mahindi na kumlawiti.
Alisema kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata mtoto huyo,
alikimbizwa Hospitali ya Mafinga wilayani Mufindi, Iringa na baadaye
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alikotibiwa kwa miezi
minane.
Akitoa hukumu baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani
hapo, Hakimu Mfawidhi Guwai Sumaye alisema anamhukumu Mnyonge kwenda
jela kutumikia kifungo cha maisha ili iwe fundisho kwa wengine wenye
tabia hiyo.
Blogger Comment
Facebook Comment