
Imeshindwa kueleweka haraka kama ni
hasira, wivu au ni kweli amesahau kabisa mapenzi ya Nicki Minaj?.
Huyu
si mwingine bali ni Safaree ambaye alikuwa Boyfriend wa female rapa
Nicki Minaj.
Safaree ametupia picha kwenye instagram
yake ambayo ameonyesha kufuta tattoo za Nicki Minaj moja ni ile iliyo
kuwa kwenye mkono wake wa kulia, na ile iliyokuwa kwenye upande mmoja wa
kifua chake.
Safaree amefuta tattoo hizo ambazo
haikutegemewa kwamba ingefutika maishani kwani ilichorwa kwa ubora wa
hali ya juu lakini hatimaye tattoo zimefutwa na kuchorwa tattoo nyingine
ya ua juu yake.
“Unafikiri ingekuwa ngumu?…nimefanikiwa,
sorry NickiMinaj” hayo ni maelezo “caption” ya picha hiyo ya tattoo
mpya mkononi yaliyo andikwa na Safaree.
Blogger Comment
Facebook Comment