Msanii wa Bongo Flava Kutoka Makambako Ambaye anafanya poa na Ngoma yake ya 'Baby Why Sajo' Mabusness a.k.a Mabusnenga Amevunja ukimya na Kuweka wazi kuwa Hawezi kufanya mziki wa kushindana na Mtu yeyote Bali anafanya Mziki Kwa starehe na kwaajili ya Wadau wake ambao wanazipokea kazi zake,Amezungumza hayo baada ya baadhi ya watu kupitia mitandao kumshindanisha na wasanii wengine kutoka Kusini,
Sajo Mabusness katika Pozi Uswahilini.
Ameeleza hayo wakati akifanyiwa Interview na kituo kimoja cha radio hapa Jijini Dar es salaam huku akiweka wazi mipango yake chini ya MKclassic Amesema kuwa Tayari yupo katika maandalizi ya kufanya Video ya ngoma yake ya' umenithibiti' ambayo amefanya kwa Mr T touch,Lakini Bado anajipanga Kuachia ngoma nyingine ambayo ameifanya katika studio za AM records chini ya pro Bob Manecky
''Sina mpango wa kufanya kazi kimashindano nafanya kazi kwaajili ya wadau wangu wanaopenda mziki mzuri si kwasababu flani katoa ngoma hii na mimi ni toe ya mtindo huu huo sio Mziki bali ni majibizano na mimi nafanya kazi chini ya menejimenti na napangiwa kila kitu cha kufanya katika mziki wangu ndio maana ngoma zangu zinafanya poa katika midea huwa spendi kuzungumza haya mambo,Kikubwa Wategemee kazi Nzuri kutoka kwangu''
Kuhusu album amesema hana mpango wa kutoa album katika kipindi cha hivi karibuni
,
Blogger Comment
Facebook Comment