Unaikumbuka Ngoma kama Ngo ngo,Nakupenda ambazo zilifanya vizuri sana na tunakumbuka aliwapa support washikaji zake Alikiba na Mr Blue na Sasa amerudi na ngoma mpya inaitwa Averina ambayo imekuwa Gumzo kitaa wadau walimmiss sana mshikaji baada ya kupotea kwa muda kidogo.
Akizungumza na
Vmix ya channel ten Abby amesema majukumu ya kimaisha yalimfanya awe kimya kidogo kwa muda licha ya kuachia ngoma kwa kipindi cha hivi karibuni lakini hazikufanya poa,Na Averila ni ngoma ambayo mwaka mmoja uliopita ilianza kutengenezwa na Nje ya Averina amesema kuwa kuna ngoma nyingine ambazo wameshazifanya wanasubiri kuziachia tu,
Amesema kuwa kunaproject kubwa ambayo wameifanya ikisimamiwa na Yeye mwenyewe ,Mr blue pamoja na Alikiba ilikufanikisha mziki wa Bongoflava kufika mbali na watu waamini kuwa amerudi vizuri katika game na kwa namna ya kipekee.
Baada ya kuulizwa na Mtangazaji wa kipindi hicho
Mwaka Ze Bwoy kuhusu kama Alikiba na Mr Blue nje ya mchango wa kimawazo wanaoutoa Je Kuna kiasi cha fedha chochote wanachokitoa Abby amesema kuwa ieleweke kuwa kila kitu wanakisimamia pia na wanamchango mkubwa katika hiyo project.
Blogger Comment
Facebook Comment