Mkclassic Production Kung'arisha na Kufanya Video Za Kimataifa za Msanii wa Gospel Asifiwe Eliazar Ndendya

Msanii wa Injili mwenye Ndoto Kubwa Katika Mziki Wa Injili Kutoka Mkoani Mbeya Anayefahamika zaidi kwa jina la Asifiwe Eliazar Ndendya Ameweka wazi uamzi wake wa kufanya video na kampuni mpya ya Mkclassic Production ilikufanya video kubwa za kimataifa na kupata ushirikiano wa usambazaji wa kazi zake Kupitia kampuni hiyo.
                                         Msanii wa Nyimbo za Injili Asifiwe Ndendya

Akizungumza na MwakaTv Amesema kuwa Malengo makubwa aliyonayonikufanya Video za kimataifa zaidi ili kushindana na Soko la Kimataifa katika mziki wa Injili na Kampuni hiyo haitafanya Video Moja Bali ni album nzima yenye Nyimbo Sita Ambazo zinaujumbe Mzuri wa kuvutia kwaajili ya wasikilizaji hivyo Imemlazimu kabisa kufanya video nzuri na zenye Ubora,

Lakini pia ameeleza kuwa Kufikia Mwezi wa kumi na mbili wataingia location na video amepanga kuifanyia katika Jiji la Dar es salaam katika maeneo mbali mbali kadri  Director atakavyopanga,Huku akieleza sababu sababu ya kufanya kazi na kampuni hii mpya ni kutaka kuleta utofauti wa video hii inatokana na ubora wa kazi katika kampuni ya Mkclassic Production.



 ''Nashukuru kampuni ya Mk Classic kwa kunikubalia kufanya kazi na wao ili kuufikisha mziki wangu mbali na kunisaidia katika kuusambaza mziki wangu kila kona ili tuweze kueneza injili ya bwana mimi naamini kwa nguvu ya Mwenyezi Mungu tutafanikisha hili jambo salama niseme tu maandalizi yakutosha yameanza na mwezi wa kumi na mbili ninaingia location kushoot album yangu mpya ambayo inanyimbo sita''amesema asifiwe
 
 Naye Meneja wa Mkclassic Bwana Immanuel Mnami amesema kuwa wanashukuru kwa sasa wanavifaa vipya vinavyoweza kupeleka video zetu katika mziki wa kimtaifa hata kama ni Gospel kwa uwezo aliotupa mwenyezi Mungu tutatangaza injili kwa Namna ya kipekee na injili itatangazwa tu kupitia mziki na video nzuri zenye mvuto kwahiyo tufahamu Asifiwe ni msanii mzuri wa injili kutokana na uwezo wake mzuri wa kuimba hakika haitatupa shida kumfanyia kitu kizuri ili tusimuangushe.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment