Msanii wa Filamu Za maigizo Tanzania ameamua kupumzika kidogo kufanya filamu na Nguvu zote ameamua kuziweka katika kufanya mziki wa bongoflava Tanzania.Amefunguka hayo wakati akifanyiwa Interview na Mwanahabari wetu Richard John kuwa ameamua kupumzika ili kujipa nafasi ya kufanya Mziki mzuri kwaajili ya watu wazuri na kuna wasanii ambao walikuwa wanaigiza na sasa wanaimba kwahiyo wanampa matumaini kuwa na yeye atafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Akizungumzia kuhusu ujio wake Mpya ameeleza kuwa kuna ngoma ambayo Inatarajia kutoka hivi karibu ambayo anategemea kufanya na msanii wa Bongo Flava Sajo Mabusness,
Baada ya kuulizwa kuhusu mpango wa kufanya kazi na Management amesema kwa sasa hayuko Tayari Kulizungumzia hili ili kupisha baadhi ya mambo mhimu yafanyike na wakati ngoma inatoka tu ndipo wadau wake watafahamu ni Menejimenti gani atakayokuwa anafanya nayo kazi,Lakini pia ameeleza kuhusu hiyo menejimenti amesema anauhakika itamfisha mbali zaidi.
''kwanza na mshukuru Mungu kwa hatua ambayo nimeipata na kuzungumza kuhusu kazi zangu kikubwa wadau wangu wategeme mambo makubwa kutoka kwangu na Kuhusu uongozi aah ninao ila nitaweka wazi hivi karibuni wakati nitakapokuwa naachia wimbo wangu mpya ambapo siku hiyo nitatambulishwa rasmi na kufanyiwa sherehe flani hivi amazing''amesema irene
Na baada ya kuulizwa kuhusu mahusiano ya kimapenzi amesema anashukuru Mungu anaye mpenzi ila ni Mapema kuweka wazi kwa kipindi hiki ila watu wafahamu kuwa tayari anaboyfriend.
''Namshukuru Mungu nimempata mpenzi na siku si nyingi nitamuweka hadharani na watu wafahamu ila ninawivu sana hahaaa' 'amesema irene
Home / Uncategories / Msanii wa Filamu Irene Swaumuh apumzika Kufanya Filamu Aingia rasmi Kufanya Mziki wa Bongoflava
Blogger Comment
Facebook Comment