Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji la dsm
hususan wafanyabiashara kutumia fursa ya Ujio wa Mfalme wa morroco wa 4
anayetarajia kuingia nchini siku ya jumapili kujenga mahusiano ya
kibiashara pamoja sekta ya utalii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dsm Bw,makonda amesema
Mfalme huyo wa morroco atafuatana na Msafara wa wafanyabiashara zaidi ya
Elfu moja ambao pamoja na mambo mengine watakutana na wafanyabiashara
wa Tanzania katika kuangalia maeneo ya uwekezaji,utalii lakini pia
usafirishaji bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Miongoni mwa mikataba itakayosainiwa kati ya Tanzania na Morroco ni
pamoja na Ujenzi wa reli kutoka kilwa hadi mtwara,mikataba ya kusaidia
sekta ya kilimo pamoja biashara.
Aidha Mkuu wa mkoa amewataka wakazi wa jiji la dsm kujitokeza kwa
wingi wakati wa ujio wa Mfalme huyo lakini pia amewataka wananchi kuwa
wavumilivu hasa pale barabara za nyerere,gerezani,sokoine na stesheni
wakati Msafara wa Mfalme huyo atakapopita.
Chanzo;Channel ten habari
Home / Uncategories / Wakazi wa jiji la Dsm hususan wafanyabiashara kutumia fursa ya Ujio wa Mfalme wa morroco wa 4
Blogger Comment
Facebook Comment