Wimbo Wa Nikupe Nini Mwili Wa Msanii Wa Nyimbo Za Injili Mhugo Hantish Watikisa Kenya,

Msanii Wa Nyimbo za injili Kutoka Tanzania maarufu kama Mhugo Hantish Ambaye hivi karibuni amefanikiwa kufunga harusi ikiwa ni ndoto ya vijana wengi kufikia hatua kama hiyo,Amekuwa miongoni mwawasanii ambao nyimbo zake zinapigwa katika media mbali mbali nchini  Kenya,

  Wimbo wa ''nikupe nini mwili'' ikiwa ni wimbo ambao umebeba jina la album yake Mpya yenye nyimbo 8 Ambayo bado inafanya vizuri sokoni na Wimbo huo umeonekana kupendwa na watu wengi nchini Kenya na Hata Ndani ya Tanzania,

Siku chache zilizopita MwakaTv ilipiga stori na Msanii Huyo kuhusu maendeleo ya album yake na ameeleza bado inazidi kufanya vizuri sokoni na anashukuru ameanza kusambaza nyimbo mpaka nchi jirani hii ni kutokana na ushirikiano mkubwa alionao na baadhi ya watu ambao wanaconnection kubwa na watu mbali mbali nje ya Tanzania.

 Kuhusu Mpango ya Video Amesema kuwa kutokana na ushindani mkubwa uliopo katika video amejipanga kufanya Video na kampuni kubwa ambayo inamilikiwa na mtu maarufu sana ingawa amesema ni  mapema kuweka wazi ila muda ukifika tutaweka wazi kila jambo ila wafahamu mpango wa kuleta video nzuri na zenye ubora upo.

Na amewashukuru wadau wake ambao wanampa support kwa kununua album yake sokoni.



Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment