Huyu ni Mtu ambaye anampa jeuri ya Mziki Don Flavour Siri Imefichuka.

Kasi ya mziki ya msanii kutoka Mbeya mkali wa ''Twende Nyumbani'' Ngoma ambayo inasumbua sana katika Media na kushika namba moja katika Media hapa namzungumzia Don Flavour aliyebarikiwa kuwa na sauti nzuri inayokubarika na watoto wa kike wengi.Huku wadau wakiisubiria Ngoma yake mpya ambayo Imetengenezwa na Producer wawili hapa namzungumzia Bob Maneck na Snaisha katika studio za Bmk Records.
                                                         Huyu ndio Boss Kid katika Pozi

Watu wengi walianza kujiuliza kuhusu mafanikio ya msanii huyo na jeuri ya kufanya mziki mzuri huku akiwa na Video Nzuri ambayo imefanywa na Director mkubwa wa Tanzania namzungumzia Msafiri wa Kwetu Studio ikiwa ni director anayekimbizana na soko la mziki Tanzania.

Akiweka mikakati yake kwa mwaka 2017 kuhusu kazi yake ya mziki amesema kuwa amejipanga vizuri na wadau wategeme Ngoma kali kutoka kwake na hatowaangusha kwasababu anasubiri ngoma yake hii mpya ikamilike aachie pamoja na Video ili wadau wapate kitu kizuri zaidi ikiwa ni zaidi ya kile cha Mwanzo.

Baada ya kuulizwa swali na mtangazaji wa kituo cha Radio hapa jijini Dar es salaam kuhusu Mtu ambaye anagharamia kila kitu na kufanya masoko ya kazi yake ya Mziki mpaka kufikia hatua ya Ngoma yake kuchezwa katika kituo kikubwa afrika nazungumzia MTVe amesema kuwa kwa watanzania jina sio geni na mtu ambaye anamsimamia Ni Bosi wake ambaye ni kijana mdogo mwenye kujituma katika kazi ambayo inambidi aifanye hapa anamzungumzia Boss Kid,Huyu ni mtu anaye Mpa jeuri ya kufanya mziki mzuri ukakubalika na watu wengi sana.

Boss kid ameweka wazi kuwa anapenda kushukuru sana Vyombo vya habari kwa support kubwa wanayoionyesha na kikubwa wategemee vitu vizuri kutoka kwa msanii wake Don Flavour,Huku akieeleza mipango ya kumpeleka msanii wake Kenya kwaajili ya kufanya Media tour ya ngoma yake hiyo mpya atakayoiachia hivi karibu.,




Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment