Namsaka Tour ya Donny Flavour Kuiweka Namsaka kwenye Tv na Radio za Afrika Mwezi March.

Donny  ajipanga kuachia ngoma nyingine mpya ikiwa ngoma yake aliyoiachia mwaka jana inaitwa 'Twende Nyumbani'Kufanya vizuri zaiidi.Baada ya kupiga stori na ukurasa huu amesema kuwa tayari ameshafanya ngoma na iko tayari hadi video na Mwezi March Tarehe za mwanzoni ataachia ngoma yake hiyo mpya aliyoipa jina la #Namsaka akiwa ameitengeneza kwa producer @Abidady.


Amesema Uongozi wake umejipanga vizuri kuhakikisha  unazunguka katika kila mkoa pamoja na nchi za afrika kwaajili ya hiyo Tour .Pia amewaweka Wazi Wadau wake kuwa kuna Ngoma itakayofata atafanya na Mr Blue Mpaka hivi sasa Mameneja wake wapo katika mazunguzo na mr blue Na makubaliano yanaelekea vizuri.

Kuhusu show amesema kuwa baada ya Ya Ngoma kutoka atafanya show katika baadhi ya mikoa kama Mwanza,Mbeya,Arusha,Iringa na mingine huku akisuburi kampuni mmoja kutoka Kenya ambayo inamhitaji katika Uzinduzi wa mwezi wa Tatu mwishoni kwaajili ya kupiga show ambapo Meneja wake yupo kwenye maongezi ya kukubaliana kuhusu kiasi cha pesa watakacho tulipa.

''Namshukuru Mungu niko na Mameneja wawili mmoja ni Mtangazaji na mwingine ni mfanyabiashara ambao kila siku wanapigana na mm najitahidi kuleta vitu vipya Mipango kwa mwaka 2017 ni mikubwa tusubiri ngoma kali tu na tour kutoka kwangu bila kusahau ngoma mpya ya namsaka tunasubiri siku ya kuiachia tu,,Amesema Donny Flavour
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment