Msanii wa Mziki wa Bongo flava kutoka Tanzania Verimund Kapinga maarufu kama Ba Johnson hivi sasa makazi yake Yakiwa Jijini Mbeya Msanii ambaye Huko Mngeta mkoani Morogoro wananchi humpokea kama mfalme hii ni kutokana na heshima aliyojiwekea wakati akiishi huko mngeta huku akitamba na ngoma zake mbili ambazo ni Faraja yangu na Rudi Nyumbani,Hivi sasa ameweka wazi mipango yake ya kufanya mziki mzuri zaidi ilikukata kiu ya mashabiki wake.
Akizungumza na Radio Magic fm iliyopo Dar es salaam amesema kuwa ameshaingia tayari studio na kufanya ngoma na producer ambaye amefanya ngoma nyingi nzuri na wasanii wakubwa kama Darasa,Timbulo,Bill Nass hapa anamzungumzia Mr T touch producer ambaye anauwezo mkubwa sana hapa Tanzania.
Aidha amesema ngoma tayari imeshakamilika kilichobaki ni kusubiria producer afanye yake na kumalizia Mixing baada ya hapo Maandalizi ya kufanya Video yataanza chini ya Management yake Mpya ambayo inamsimamia hivi sasa.
Kuhusu Jina la Uongozi wake mpya kuweka wazi amesema ni mapema mno baada ya kazi kutoka watajua ni nani mwenye nguvu ya kuuupeleka mbali mziki wangu ikiwa hivi sasa wapo katika mazungumzo na Wasanii wawili Mr Blue na Nandy kwaajili ya collable.
''Ki ukweli namshukuru Mungu kwa Hatua niliyofikia sio kazi nyepesi ni ngumu na sasa nimeamua kufanya mziki nitafanya mziki na nashukuru pia management yangu mpya kwa support kubwa wadau wakae mkao wa kula na wataniona kwenye matamasha makubwa hivi sasa'' Amesema Ba johnson
Home / Uncategories / Ba Johnson Atua Kwa MrT Touch Jikoni na Kupika vinavyopikika,Collable na Mr Blue Yanukia.
Blogger Comment
Facebook Comment