Filamu ya Best Player inapatikana sasa kupitia Youtube.Wamiliki wa Filamu hii wapo katika mazungumzo na kituo cha Tv cha Sinema Zetu.

Kampuni ya Bmk Production imeshaiachia Filamu iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu na wadau ikiwa imewahusisha wasanii  wanaofanya vizuri katika kiwanda cha filamu Tanzania huku wakibeba uhusika,Best player ni filmu ambayo inamilikiwa na kijana Bmk Theonestre inamuelezea kijana mmoja ambaye baada ya wazazi wake kufariki alibadilika kitabia na kuwa kijana anayependa wanawake baada ya kushawishiwa na marafiki wasiokuwa na tabia njema.

Wahusika katika film hii ni Bmk Theonestre,Mwaka Ze Boy,Bi Ndoza,Amina Abdul,Tabitha Mussa ni wahusika ambao wameweza kuipamba filamu hii ambayo mpaka hivi sasa imewekwa katika mtandao wa youtube,Kuhusu kuwekwa katika mtandao wa youtube mmoja kati ya wahusika wa filamu hii amesema wametaka kila mmoja aione  bila gharama yeyote huku maandailizi ya kuiweka katika CD yakiendelea ambapo itauzwa.

Mmoja ya wahusika Mwaka Ze Boy wakati akizungumza na Channel ten Tv na radio Magic fm amesema haiku rahisi sana kufanya filamu hii kutokana na changamoto mbali mbali zilizojitokeza huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa upande wake kufanya filamu Huku akiweka wazi kuwa hivi sasa yupo katika mazungumzo na kituo cha Televisheni cha Sinema Zetu ili filamu hiyo irushwe katika Televisheni hiyo.

Mpaka hivi sasa wadau wanaweza wakaingia youtube na kudowload movie ya best player na kuangalia ni mambo gani ambayo yalifanyika na makubwa


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment