Baada Ya Filamu Ya Best Prayer kufanya vizuri Kampuni ya BMK Production Kuandaa Filamu Nyingine.

Filamu ya Best Prayer Ni miongoni mwa Filamu ambazo zimefanya Vizuri Kwa Mwaka 2017 Filamu ambayo inaelezea maisha halisi ya Muafrika pindi anapokutana na changamoto za kimaisha baada ya kuwapoteza wazazi wake.

Kampuni ya Bmk Production imeweka wazi Mipango yake ya kuingia Location na kufanya Filamu nyingine itakayoteka Soko la Filamu Tanzania Akizungumza na Channel Ten Tv, Msanii Aliyehusika katika Filamu ya Best Player Mr Bmk Theoneste amesema kuwa Wamejipanga vizuri kuhakikisha Wanawaletea wadau wa Filamu nchini Tanzania Filamu Nzuri zenye Ushindani mkubwa katika soko la Filamu Dunia,

Amesema Anashukuru mpaka hivi sasa Meneja Wa Kampuni hiyo ambaye Yuko Tanzania anaendelea Kuongea na Wasanii wakubwa kama Jackline Wolper,Johari,Jb, na wengine ambao wataweza kuipamba Filamu hiyo mpya,

Katika Hatua Nyingine ameishukuru Serikali ya Mheshimiwa Rais  John Pombe Magufuli kupitia Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyemba Kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia  haki wasanii wa Filamu Tanzania na kuongeza kuwa Anaamini soko la filamu Tanzania litakuwa,.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment