
Ajiboye Oluwaseyi (37), Mkazi wa mji
wa Ondo huko nchini Nigeria amekamatwa na Polisi na kutupwa ndani baada
ya kushtakiwa kwa kosa la ubakaji kwa watoto wake.
Kwa mujibu wa Mama wa watoto hao,
amesema yeye na mume wake waliachana tangu mwishoni mwa mwaka jana 2014,
hivyo mume wake aliamua kuondoka na watoto hao ambao wawili ni watoto
wake mwenyewe na mmoja ni mtoto wa baba mwinginge yani mtoto wake wa
kambo.
Msemaji wa Polisi wa mji wa Logos DSP
Patricia Amadin, amethibitisha kukamatwa kwa Baba wa watoto hao, ambao
mmoja ana miaka 4, mwingine 6 na mtoto wake wa kambo ana miaka 15.
Vipimo kutoka kituo cha afya vimetoa
ripoti yake ambapo imethibitisha kwamba ni kweli watoto hao walifanyiwa
kitendo hicho cha kinyama mara kadhaa.
Mama wa watoto hao alipewa taarifa na
majirani kwamba huenda mzazi mwenzake alikuwa anawabaka watoto wake
kwani mwenendo wake ulikuwa haueleweki ambapo muda mwingi alikuwa
akijifungia ndani na watoto wake.
Mama alipata nafasi ya kuongea na moja
kati ya mtoto wake ambapo alimwambia ukweli kwamba Baba yao alikuwa
anawafanyia kitendo hicho, ndipo hapo Mama huyo alipokwenda kustaki
polisi.
Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa na huenda Baba huyo akakumbana na adhabu ya kifungo cha maisha gerezani.