
Ni muda sasa Walimu nchini Kenya wapo kwenye mgomo kushinikiza serikali kuwalipa nyongeza ya mishahara wanayoidai kwa serikali.
Kutokana na hilo serikali imelazimika kufunga shule hizo huku ikitafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Hata hivyo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amelihutubia taifa Jumapili wiki hii, akisema kinagaubaga kuwa serikali ya nchi hiyo haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo.
Rais Kenyatta ametolea wito wadau wote wa elimu nchini Kenya kuketi kwenye meza ya mazungumzo kwa faida ya taifa na wanafunzi ili kuweza kutafutia suluhu mgogoro huo, ambao ametaka utatuliwe kwa amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia Jumatatu wiki hii.
Chama cha walimu nchini Kenya KNUT kimefahamisha kuwa tayari kimepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali kuanzia jumatatu wiki hii.
Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amesema haina pesa za kuwaongezea walimu mshara, huku Wizara ya elimu ikisema mitihani ya kitaifa ya darasa la Nane na Kidato cha nne itaendelea kama ilivyopangwa, na uzinduzi wake ulifanyika Ijumaa wiki iliyopita.
Chanzo – rfi.fr
Blogger Comment
Facebook Comment