Wakati anafanyiwa Interview na Mwaka Tv Amesema alikuwa kimya kutokana na matatizo madogo na changamoto za kimaisha na anashukuru Mungu amemsaidia na kuinuka tena kuendelea na huduma ya uimbaji kama mwanzo.Amesema kuwa Tayari anajiandaa yeye na Meneja wake huyo kuachia wimbo wake mpya unaitwa ''tutashinda tu'' ambao anatarajia kuutoa mwezi Januari Mwaka 2017.Amesema ni wimbo mkubwa ambao utawashika watu wote kutokana na ujumbe mzuri uliopo katika wimbo huo.
Aidha amesema kuwa Mwimbaji aliyemvutia katika huduma ya uimbaji Ni msanii Bahati bukuku ambaye ni kwa muda mrefu amekuwa akimfatilia na hata kesho angetamani kumshirikisha katika wimbo wake.Uandishi mzuri wa nyimbo zake Bukuku ndio ulimfanya akubali zaidi kazi zake.
Mwisho amewataka Wadau wake wakae mkao wa kula kumpokea tena katika mziki na sasa amewaandalia vitu vizuri na kikubwa ni kukaa karibu na Radio,Tv pamoja na magazeti,Pia amesema anamshukuru Meneja wake ambaye anatarajia kufanya Mambo makubwa pamoja na wale wote wanaomshauri kwa kila hatua bila kusahau familia yake Baba na Mama.
Blogger Comment
Facebook Comment