Love Mo Njiani kuwakutanisha Mastaa wawili wanao sumbua Tz Mr Blue pamoja na Darasa katika Ngoma Tofauti

Msanii Daniel George Mkola maarufu kwa jina la Lovemo Ni Miongoni mwawasanii ambao wameamua Kuupeleka mbali zaidi mziki wa Bongoflava katika nchi jirani ya Zambia ili kufikia malengo yake ya Nchi jirani kusikiliza zaidi mziki wa Nyumbani kutoka Tanzania.

Ikiwa sasa Tanzania imekuwa ni miongoni mwa Nchi ambazo zinafanya vizuri katika soko la mziki Afrika na kufikia hatua ya kuchukua tuzo mbali mbali na sasa wasanii wachanga nao hawalali wanazidi kutafuta masoko ya nje ili kuzidi kuutanua mziki wetu wa Bongoflava

Lovemo msanii ambaye ameachia ngoma yake mpya ambayo inaitwa Nirudie ambayo amerap katika hii ngoma ambayo amemshirikisha msanii mwenzake Ajuxy boy Ameesema kuwa ikiwa anaishi nchini Zambia bado ananafasi kubwa ya kufanya mziki na kuutangaza mziki wake ikiwa itakuwa ni njia moja wapo ya kukitangaza kiswahili na Kuelimisha jamii.

Amezungumza hayo wakati akihojiwa  na #MWAKATV ya jiji Dar es salaam kwa njia ya simu huku akiwataka wadau wake wakae mkao wa kula anatarajia kufanya collable na wasanii kutoka Tanzania ambaye ni Darasa na Mr blue ikiwa hawa ni miongoni mwa rapa ambao anawakubali,

Mwisho amemshukuru Dada yake Divakente kwa support nzuri ya ambayo anampa kwa kumpa connection na baadhi ya watu ambao wanasupport mziki.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment