Kampuni ya EyePicture Ya Ng'arisha Kichupa huku Brana Radium Akili kuwa Ukimya Wake katika Mziki Ulimfanya Akose Raha.

Msanii Wa Mziki wa Bongoflava kutoka kusini Ambaye anatamba na Ngoma yake ya Nimejifunza Brana Radium Ametoa Yake ya Moyoni Baada ya ukimya wa Muda mrefu.Ukimya wake uliomfanya akose Raha kutokana na wadau wake Wengi kumuuliza maswali ya kila aina kuhusu mziki wake wengi wao wakiamini kuwa ameacha mziki na kufanya shughuli nyingine.

Baada ya Kufanyiwa Interview Na Magicfm zikuchache zilizopita alisema kuwa Na sasa ameamua kurudi Rasmi katika Game ili arudi katika nafasi yake ile ile ya Mwanzo Ambayo alikuwa anaishikiria Mwanzo.Hata hivyo Amesema kwasasa Anafanya Kazi chini ya Uongozi na Meneja Wake Immanuel Mnami Ambaye yuko Mwanza kwaajili Ya Nimejifunza Tour ili kuipeleka mbali ngoma ya Nimejifunza.

Akizungumzia Kuhusu Kuchelewa Video yake ya Nimejifunza Brana Radium amesema kampuni ambayo amefanya nayo kazi ya EyePicture Production ilikuwa imeshakubaliana na Meneja wake ila Mwisho wa Siku Cameramani Ngoti Yunus alisafiri na kuelekea South Afrika Ili kuchukua Baadhi ya Vifaa Vya Kushoot Video yake Hivyo ilipelekea kuchelewa Video yake.

Kuhusu Malengo yake Brana Radium ameeleza kwasasa anamuachia Meneja wake Immanuel Mnami ambaye anaongea na msanii mkubwa kutoka hapa Tanzania kwaajili ya kufanya Collable,

Mwisho amewashukuru wadau wake na kuwapa moyo wa kusubiri video yake na kwamba kichupa wameshashoot tayari kiko production bado tu Muda Ukifika Uongozi utatoa taarifa lini kichupa kitoke.

Brana Radium akiwa na Video Queen wa Nimejifunza katika Pozi



Brana radium katika pozi 
Video Queen


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment