Ni ukweli usiopingika kuwa ukiwa na kipaji ni kama umejua kuendesha baiskeli zaidi utaanza kuongeza mbwembwe za kuachia mikono na kuongeza spidi.Hii ikimaanisha kuwa kama unajua unajua tu labda wakutoe kichwa.Hivi ndivyo inavyojitokeza kwa mtangazaji maarufu Kusini Namzungumzia Regina kasiani ambaye ni mtangazaji wa Radio Ice fm ya Makambako mkoani Njombe.
Licha ya kuwa ni mtangazaji mzuri ameamua kuwaonyesha watanzania kuwa anauwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa katika Tasnia ya Filamu Tanzania,Amesema kuwa toka muda mrefu alitamani kuigiza na kuingiza sokoni filamu anazofanya ili ziweze kumlipa na kupeleka ujumbe katika jamii na sasa amesema muda umefika wa kuhakikisha anaipeleka mbali sanaa ya Filamu Tanzania,
Akielezea changamoto ambazo zilimfanya ashindwe kujikita zaidi katika filamu amesema kuwa Ratiba ya kazi yake na majukumu ya kifamilia ni vitu ambavyo vilikuwa vinamkosesha nafasi ya kufanya vizuri zaidi katika soko la filamu Ila kwa sasa amesema kuwa yuko tayari kujikita zaidi katika filamu.
Akielezea filamu ya Neria amesema kuwa ni filamu ambayo inaelezea vitu vingi ambavyo vinajitokeza katika jamaii hivyo wadau wasisite kuitafuta na kuitazama filamu hii ambayo inagusa maisha ya watu wengi zaidi.
Kwa Upande mwingine amesema wadau wasisite kujitokeza katika Tuzo kubwa Kusini za NyotaAwards Ambazo zinatarajiwa kufanyika Tar 14-5 Mwaka huu Makambako katika mkoa wa Njombe katika ukumbi wa Midtown
Mwisho amesema ni wakati wa kusubiri vipindi bora vya radio pamoja na kazi nzuri za filamu,Kuhusu Mahusiano ya kimapenzi amaesema yeye huwa hapendi kuweka mahusiano yake wazi kiufupi yeye ni msiri kwa mambo yake binafsi.
Home / Uncategories / #NyotaAwards-Regina Kasiani Mtangazaji Ambaye anaamini katika kipaji chake cha Kuigiza,Neria Ndio Filamu inayompa jeuri.
Blogger Comment
Facebook Comment