#NyotaAwards-Sajo Mabusness Amtafuta Mchawi,Ajiandaa Kutumbuiza katika Tuzo Hizo.

Msanii wa Bongoflava Kutoka Tanzania Lusajo Kunyumba maarufu kama Sajo Mabusnness mkali wa Ngoma kama Umenithibiti amesema kuwa Umefika wakati wa kutoa Makucha yake katika Kuonyesha uwezo wa Kuperform katika stage mbali mbali ambazo atapata nafasi ya kuzimiliki kwaajili ya kuwapa burudani wadau wake.
                              Sajo Mbusnnes kwenye Pozi
Akizungumzua Nafasi ya Mualiko aliyoipata kutoka kwa waandaji wa tuzo hizo za Nyota Awards zinazotarajiwa kufanyika tarehe 14 mwezi huu katika Ukumbi Wa Midtown Mkoani Njombe Amesema kuwa anaheshimu Mawazo ya waandaji na hii inaonyesha ni jinsi gani mziki wake Unathaminika na ndio maana wametambua umhimu wake katika Tuzo Hizo.Pia ameshukuru Uongozi wa Radio Icefm Ya Makambako ambao ndio wadhamini  wakubwa wa Tuzo hizo.

Kuhusu Maandalizi ya Mziki wake amesema kuwa Siku zote Maandalizi yanafanyika kwa hiyo wadau wa kusini wategemee vitu vizuri kutoka kwake siku hiyo na waende kuunga mkono Tuzo hizo Ambazo anaamini zitaleta Mapinduzi Makubwa zaidi katika Mziki wa kusini.

Mwisho amesema kuwa Wadau wake wakae mkao wa kula baada ya Umenithibiti kuna balaa lingine linakuja kutoka kwake ambalo ni kama kishindo cha Kiboko.




Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment