#NyotaAwardsNjombe-Ni Tuzo Za Kuzitazama Mara Tatu Na Kwa Jicho Tofauti Kabisa,Wasanii Kusini Wapata Changamoto.

Tuzo ni heshima kubwa katika Jamii kupitia jambo fulani unalolifanya na jamii inanufaika vipi,Njombe ni mkoa mpya ambao unakuja kwa kasi katika maswala mbali mbali kuanzia Elimu,Biashara Pamoja na burudani.Hili jambo sio la kawaida Miongoni mwawatu walitafsiri kuwa hawa waandaaji wanapoteza muda Bila kujua nini lengo lao na ni jinsi gani wamejipanga kufanya mapinduzi makubwa katika mziki.

Kama ni mfatiliaji mzuri wa mitandao naamini utakuwa umekutana na pilika pilika za wasanii mitandaoni wakiomba kura kwajili ya kushinda Tuzo ambazo zimedhaminiwa na kituo cha radio Ice fm,

Mwaandishi wetu amepiga stori na mtangazaji Gami Dee ambaye anafanya kazi katika kituo hicho amesema kuwa huu ni wakati wa kuwasogeza wasanii wachanga na wasanii kutoka kusini pamoja na Tanzania kiujumla katika mziki wa kimataifa na kuwapa moyo,Lakini si kwa ajili ya hawa tu bali ni kwaajili ya wasanii wote wa mziki wa bongoflava.

Mwisho amesema Wadau wote wapenda burudani wasikose kufika siku ya tarehe 14-5 mwaka huu ambapo Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Midtown Mjini makambako katika Mkoa wa Njombe.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment