Njombe Waipokea Singeli Flava kutoka kwa Brana Radium Ikiwa Maalumu Kwaajili ya Timu ya Njombe Mji

Msanii Kutoka Njombe Brana Radium mkali wa Nimejifunza  ameamua kuja na Kitu cha kipekee Baada ya Timu yake ya Nyumbani Kupanda daraja,Kutokana na  Timu ya Njombe Mji kupanda daraja Yeye pamoja na uongozi wake Wakaamua kuingia Studio ili wafanye ngoma kwaajili ya Wadau wa Timu ya Njombe Mji.

Mpaka hivi sasa Mapokezi yamekuwa mazuri Huku wakijipanga katika maandalizi ya Video ambapo uongozi wake Umesema ili kuonesha  Uzalendo zaidi Video itafanyika Njombe na Director Kutoka Njombe,

Naye Msemaji wa Klabu ya Njombe Mji Bwana Mhagama ameshukuru hatua aliyoifikia msanii huyo na kuomba wadau wajitokeze kuhakikisha wanatoa sapoti katika kufanyika Video ya Ngoma hii.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment