Fri Cee Aweka wazi Mipango yake ya kufanya Ngoma na Producer Mkubwa Tanzania na Mipango Ya kumuweka karibu Jackline wolper,

Msanii Mpya wa mziki wa Bongoflava ambaye anaishi U.S.A  anafahamika kwa jina Fri Cee Ameweka wazi Mipango yake ya Kutoa Ngoma mpya Mwaka huu Mapema na Matarajio yake ni Kufanya Ngoma na Producer mkubwa kutoka Tanzania Ambaye anafahamika kwa jina la Mr Ttouch Ambaye ametengeneza ngoma kali ya Darasa inaitwa Mziki Nngoma  Ambayo ilisumbua sana Mwaka Jana na ilikuwa ni wimbo wa taifa Ukizungumzia  mziki wa bongoflava kutoka Tz.


Fri Cee Amesema ili Kunogesha Mziki wake anatarajia kuufanya wimbo wake Mpya kwa Lugha ya Kiswahili ikiwa Atakuwa karibu na msanii killy ambaye anasifika katika uandishi mzuri wa Mashairi ikiwa ameshawahi waandikia mastar wakubwa kutoka Tanzania na Kenya,Killy anatamba na ngoma ya Nikwambie inayoshika nafasi za kwanza katika Media Mbali mbali Africa,

Amezungumza Haya Kupitia Radio Moja Nchini Tanzania kuhusu Mipango yake,Na Kuhusu Kumpost Mara Kwa Mara Star wa filamu kutoka Tanzania Jackline Wolper  ambaye anafanya vizuri katika soko la filamu kwenye Mitandao ya Kijamii  Amesema kuwa ni Msanii ambaye anamkubali sana na Anatarajia ipo siku akamtumia katika Ngoma yake Mpya kama video Queen Endapo Watakubaliana katika hii kazi ambayo anatarajia kuiachia Muda si Mrefu.

Video Ni kitu Mhimu Kutoka kwa wasanii kwasababu zimekuwa zikiwatambulisha mbali zaidi kimziki Amesema kuwa Meneja wake aliyoko Tanzania anampango wa kuongea na Director Msafiri Ilikuleta Utanzania Zaidi.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment